Dec 1, 2012

Rufaa kusikilizwa na majaji Salum Massati, Katherine Oriyo na Nathalia Kimaro.

RUFAA ya kupinga hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam iliyompa ushindi Mbunge wa Ubungo, John Mnyika katika kesi ya uchaguzi dhidi yake, sasa imeiva.
Tayari rufaa hiyo imeshapangiwa jopo la majaji watu wa Mahakama ya Rufani watakaoisikiliza na kuitolea uamuzi na imepangwa kusikilizwa wiki ijayo.
Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya Mahakama ya Rufani, rufaa hiyo imepangwa kusikilizwa Desemba 7 mwaka huu.
Ratiba hiyo inaonyesha kuwa rufaa hiyo itasikilizwa na majaji Salum Massati, Katherine Oriyo na Nathalia Kimaro.
Rufaa hiyo ilifunguliwa Oktoba 25 mwaka huu na aliyekuwa mgombea wa ubunge katika Jimbo la Ubungo kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hawa Ng’humbi, aliyekuwa mlalamikaji katika kesi ya msingi.
Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyotolewa na Jaji Upendo Msuya Mei 24, 2012, ilitupilia mbali madai ya Ng’humbi ikisema alishindwa kuyathibitisha na badala yake, ikamthibitisha rasmi Mnyika kuwa mbunge halali wa jimbo hilo. Hata hivyo, Ng’humbi hakukubaliana na hukumu hiyo, ndipo akakata rufaa akiiomba hukumu hiyo itenguliwe.
Ng’humbi anayewakilishwa na Wakili Issa Maige, katika rufaa yake hiyo ameorodhesha hoja 10 za kupinga hukumu hiyo, akidokeza kile anachokiona kuwa ni udhaifu katika hukumu hiyo.
Pamoja na mambo mengine, Ng’humbi anadai kuwa Jaji aliyesikiliza kesi ya msingi na kutoa hukumu hiyo, alikosea katika kutafsiri sheria na kupima ushahidi wa pande zote.
Ng’humbi anadai kuwa jaji alikosea kisheria na kiukweli kwa kusema kuwa makosa yaliyobainika katika ujumlishaji na kuhesabu kura na kusababisha kuwapo kwa kura 14,854, zisizohesabiwa hayakuathiri matokeo ya uchaguzi.
Anadai kuwa aliweza kuthibitsha kuwapo kwa makosa katika mchakato wa uchaguzi yaliyosababisha kuwapo kwa kura 14, 854 zisizohesabiwa na kwamba jaji alikosea kisheria na kiukweli kwa kutokuhamishia kwa mdaiwa, jukumu la kuelezea sababu za kuwapo kwa dosari hizo.
“Jaji alikosea kisheria na kiukweli kusema kwamba kura 14,854, ambazo hazikuhesabiwa zilitokana na makosa ya kibinadamu, bila kuwepo na ushahidi kuhusu hilo katika kumbukumbu za mahakama.”
Katika hoja nyingine, Ng’humbi anadai kuwa jaji alikosea kisheria na kiukweli kwa kusema kuwa hazikutumika kompyuta ambazo hazikuwa zimeidhinishwa na mamlaka husika katika kujumlisha na kura.

Jaji Mkuu: Siku ya kesi ya Lema nitakuwa nje ya nchi, sijajitoa



JAJI Mkuu, Mohamed Chande Othman ameeleza sababu za kutokuwa kwenye jopo la majaji waliopangwa kusikiliza kesi ya aliyekuwa mbunge wa Chadema mkoani Arusha, Godbless Lema.
Jaji mkuu, alitoa maelezo haya jana alipozungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu kwenye mahafali ya 12 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA).
“Ngoja nitolee ufafanuzi suala hilo ili jamii itambue utaratibu wa uendeshaji wa Mahakama ya Rufani, ambayo ina majaji 16 nchini,” alisema Jaji Othman.
Jaji Othman alisema kimsingi hajajitoa kushughulikia kesi hiyo, ila siku ambayo kesi hiyo inatajwa, atakuwa nchini India kuhudhuria Mkutano Mkuu wa 13 wa Majaji Wakuu Duniani.
Maelezo hayo ya Jaji Chande yamekuja siku tatu baada ya gazeti hili kuripoti kuwa, mkuu huyo wa mhimili wa Mahakama nchini amejitoa kusikiliza kesi hiyo na nafasi yake imechukuliwa na Jaji Bernard Luanda.
“Kwanza ifahamike kwamba, jaji wa Mahakama ya rufani hana ubia na kesi yoyote kwa mujibu wa utaratibu. Jaji yeyote kati ya majaji 16 wa mahakama ya rufani nchini ana mamlaka ya kusikiliza kesi yoyote ya rufani,” alieleza Jaji Othman.
Jaji Othman alifafanua kuwa, rufani ya Lema ni miongoni mwa kesi tatu za uchaguzi zilizobaki ambazo kwa mujibu wa taratibu za kisheria, huanza kusikilizwa baada ya muda wa mwaka mmoja na hukumu yake ni lazima itolewe ndani ya mwaka mmoja tangu kuanza kwake.
“Hivyo basi, kwa vile Jaji yeyote wa Mahakama ya Rufaa anaweza kuisikiliza kesi hiyo, hakukuwa na sababu inisubiri mimi,” alisema.
Jaji Othman alitaja kesi nyingine za uchaguzi zitakazoanza kufanyiwa vikao vya rufani na jopo la majaji wa Mahakama ya Rufani kuwa, ni ile ya Jimbo la Ubungo kati ya Hawa Ng’umbi na John Mnyika ambayo itakuwa chini ya jopo la majaji watatu; Jaji Nathalia Kimaro, Jaji Salum, Salum Masati na Jaji Katherine Oriyo.
Nyingine ni ya Jimbo la Ilemela ya Yusuph Yussuph Masengela Lupilya na wenzake wawili dhidi ya Highness Kiwia na wenzake wawili, ambayo itakuwa chini ya jopo la Majaji Januari Msofe, Jaji Beard Luanda na Jaji Salum Massati.
Alisema rufani ya Lema haijaanza kusikilizwa kwa jaji yeyote, hivyo yeye asingeweza kujitoa kwa kuwa hajapangiwa.
“Kinachotatiza hapa ni kwamba, watu wanaifungamanisha rufani hii na ile ya Arusha ambayo mimi nilikuwa miongoni mwa jopo la majaji kama mwenyekiti.

UZINDUZI WA ALBAM YA MASHUJAA NA JB MPIANA YAINGIA DOSARI.....MMILIKI AZIMIA NA KUKIMBIZWA HOSIPITALI


Watu  mbalimbali wakiwa wamelizunguka jenereta leo usiku
  Mwanamuziki kutoka DRC-Congo,JB Mpiana akitumbuiza jukwaani mara baada ya kupanda mnamo majira ya saa tisa kasoro,baada ya hitilafu za umeme kwenye jenerata kurekebishwa.
-------------------------
SHOO YA UZINDUZI WA ALBAM YA PILI YA MASHUJAA BAND, ILIINGIA DOSARI NA KUTAKA KUSHINDWA KUFANYIKA  KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB USIKU HUU KUTOKANA NA KATIZO LA UMEME LA MARA KWA MARA LINALOSABABISHWA NA JENERETA LINALOTUMIWA KUTOA UMEME KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB,JIJINI DAR.

HALI HIYO ILIPELEKEA MMILIKI WA BENDI YA MASHUJAA,MAMA SAKINA KUPOTEZA FAHAMU NA KUKIMBIZWA HOSPITALI.

UBUNGE NI KAZI YA KIBWEGE..." AFANDE SELE KATIKA XXL JANA

Ubunge ni kazi ya 'kibwege' watu wamekuchagua ili uwatumikia kwa hiyo unatakiwa kuwa mtumwa wa watu wako kwa kuwa karibu na kufanya kile wanachokihitajiwao na siyo kukalia kiti hicho kwa niaba yako na ndugu zako, inanishangaza sana mtu anachaguliwa ndani ya miaka miwili tayari anamiliki Vogue sasa huu ka siyo wizi ni nini" Afande Sele