Oct 24, 2012

HATIMAYE H.BABA AMLIPIA MAHALI FROLA MVUNGI



ULE uchumba uliodumu kwa muda mrefu kati ya mastaa filamu na muziki wa Bongo Fleva nchini, Hamis Baba ‘H. Baba’ na Flora Mvungi umefikia pazuri baada ya H – Baba kumtolea mahari na kumvalisha pete ya uchumba.

H-Baba akimvisha pete ya uchumba, Flora Mvungi.
Tukio hilo lililokuwa na mvuto wa aina yake lilichukua nafasi juzi Jumamosi, katika Ukumbi wa The Atriums Hotel, Sinza – Afrika Sana, Dar na kuhudhuriwa na ndugu wa pande zote mbili.


Kinyume na ilivyozoeleka, zoezi la kutoa mahari kufanyika nyumbani, kwa wawili hawa ilikuwa tofauti kwani kila kitu kilimalizikia ukumbini humo.

H-Baba akiwasalimiana ndugu na jamaa.
Kwanza lilianza zoezi la makabidhiano ya mahari, kisha ndipo H – Baba akaruhusiwa kumvalisha Flora pete ya uchumba, tendo lililoamsha shangwe na vigelegele ukumbini humo.

Flora Mvungi kabla ya kuvishwa pete ya uchumba.

“Namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kufanikisha tukio hili, japokuwa gharama ilikuwa kubwa lakini niliweza kujitutumua mwenyewe bila kuomba mchango kwa mtu yoyote.....Alisema H baba  na kuongeza:


“Jambo kubwa ninalotamani litokee na ninaamini litafanikiwa ni kufunga ndoa na Flora wangu. Ninampenda sana na nina uhakika na uchaguzi wangu.”H-BABA



Baadhi ya mastaa waliohudhuria ni pamoja na Baby Madaha, Kulwa Kikumba ‘Dude’,  Hisani Muya ‘Tino’, Jacqueline Dustan ‘Jack wa Maisha Plus’, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Husna Idi ‘Sajenti’ na Wilson Makubi aliye Katibu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF).

Ndugu na jamaa waliohudhuria tukio hilo.
H-Baba akiwasalimia wageni waalikwa.

ULIMI HAUNA MFUPA....ALILOLIFANYA NAIBU WAZIRI WA ELIMU NI KOSA LA KIBINADAMU.SOTE HUPITIWA..!!!




Mheshimiwa Philipo Mulugo
Siku chache zilizopita, naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Mheshimiwa Philipo Mulugo alikuwa nchini Afrika Kusini kuwasilisha mada kwenye mkutano uliopewa jina la ‘Education for Employment, Developing Skills for Vocation at the Innovation Africa’ na kufanyika October 5 hadi 7 katika hoteli ya Westin Hotel, Cape Town.


Mkutano huo ulidhaminiwa na serikali ya Afrika Kusini na kuandaliwa kwa ushirikiano wa AfricanBrains na chuo kikuu cha Western Cape.

Awali akiongea kwa ‘kutojiamini’ naibu waziri huyo alijikuta akijichanganya pale aliposema, “Tanzania was formed in 1964 by unifying the Indian Ocean Islands of ‘Zimbabwe’ and Pemba and the mainland country formerly known as Tanganyika.

angekumbuka amesema nini angerekebisha kuwa alimaanisha Zanzibar na sio Zimbabwe.

Mara ngapi ulishawahi kujikuta umeongea kitu kwa makosa na kusahau kuwa umekosea mpaka mtu mwingine akuambie umekosea?

Kumekuwepo na mijadala mingi kuhusu hotuba hii huku wengi wakianza kumhukumu naibu waziri kuwa alimchemka kwa kutoijua vizuri nchi yake.