Oct 25, 2012

KICHANGA CHAOKOTWA KIKIWA KIMETUPWA CHINI YA MLIMA KIVES




Baadhi ya wananchi waliojitokeza kuuangalia mwili wa kichanga hicho
Hizi ni picha tulizozipata kwenye mtandao wa Jamii Forum zikiwa na maelezo: MAJONZI, HUZUNI, NA SIMANZI ZIMETAWALA LEO MAENEO YA KIJENGE JUU KATA YA KIMANDOLU ILIYOKO MKOANI ARUSHA BAADA YA KITOTO KICHANGA KUKUTWA KIMETUPWA CHINI YA MLIMA KIVESI. 

Hakuna maelezo kuwa kichanga hicho kinekutwa hai kwakuwa mtu aliyeweka picha ametumia maneno kama ‘mwili’ wa mtoto huyo kumaanisha kuwa hakuwa hai. .

Mtoto mwenye umri wa siku moja wa jinsia ya kike akiwa amewekwa kwenye ndoo na kutupwa


Afisa wa polisi akiuchukua mwili wa mtoto huyo uliofungwa na kanga na kutolewa na msamaria mwema muda mfupi baada ya kutaarifiwa kuhusu tukio hilo

MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOA WA MBEYA MH. DK MARY MWANJELWA ATEMBELEA KABURI LA KATIBU WAKE NA KUTOA POLE YA KIASI CHA SHILINGI MILION MOJA WILAYANI ILEJE MBEYA

Mheshimiwa mbunge viti maalumu mkoa wa Mbeya Dk Mary Mwanjelwa akilia juu ya kaburi la katibu wake Amina Mwashambwa alieteketea kwa moto katika ajali iliyotokea mwezi uliyopita mbalizi mbeya mweshimiwa mbunge alienda kuhani msiba huo huko ileje

MADEE AJITOA TIP TOP CONNECTION


MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya anayewakilisha pande za Manzese,

 Hamad Ally ‘Madee’, kutoka kundi la Tip Top Connection, inadaiwa kuwa 

amejitoa katika kundi hilo, na sasa anataka kufanya muziki kivyake na sababu za kujitoa kwake bado hazijulikana.

Chanzo chetu cha habari kilichozungumza nasi
, kwa sharti la kutotajwa kwa jina lake kilidai kuwa wiki iliyopita msanii huyo alikuwa kwenye mzozo na mmoja wa wasanii wa kundi hilo lakini waliweza kupatana ingawa jamaa bado anaonekana kutopenda kile kilichotokea lakini bado kuna vitu vingine vya ndani zaidi vilivyosabisha hadi jamaa kuamua kujiweka pembeni.

Chanzo hicho kilichopo karibu na wasanii hao hakikusita kueleza kuwa ndani ya kundi hilo kuna matatizo mengi, kwani hata kuondoka kwa baadhi ya wasanii waliokuwa hapo kulisababishwa na matatizo hayo ambayo yamemfanya Rais huyo manzese kujiengua, ingawa bado kuna mvutano mkubwa unaoendelea ili kumrudisha kundini jamaa huyo bila taarifa za mkwaruzano huo kutoka nje.