Aug 12, 2012

MJUE STAA WETU WA LEO!!!

ROBIN VAN PERSIE

Jina kamili anaitwa Robin Van Persie wengi hupenda kumwita RVP, alizaliwa tarehe 6 august 1983, Uholanzi, ana urefu wa futi 6 na inchi 2. Mama yake anaitwa Jose Ras ambaye ni mchoraji na baba yake ni mchonga vinyago. alizaliwa katika nyumba ya wasanii lakini yeye hakutaka kuwa kama wazazi wake hivyo kipaji chake kilijidhihirisha wazi katika mpira wa miguu. ana dada zake wawili Lilly na Kiki jumla kwao wako watatu akiwa ni mtoto pekee wa kiume. 
      Akiwa na umri wa miaka kumi na saba alijiunga na timu ya vijana SBV Excelsior's youth squad mwaka 2001, lakini haikumchukua muda mrefu aliondoka katika timu hiyo mara baada ya kukosekana maelewano na kocha wake hivyo kujiunga na Feyenoord kwa mkataba wa miaka miwili na nusu. Akiwa na timu hiyo alipata tuzo ya KNVB ya kijana mdogo mwenye kipaji mwishoni mwa mwaka 2001/02. Lakini pia hapakuwa na melewano mazuri na kocha wake Bert Van Marwijk hivyo kufanya Van kukaa benchi muda mrefu
     alisaini mkataba mwingine wa mwaka mmoja na Feyenoord 2003/04, hata hivyo bado aliendelea kukaa benchi muda mrefu, ingawa katika mechi alizocheza alifanikiwa kufunga magoli 28 tu yakiwa ni magoli machache sana ukilinganisha na magoli aliyofunga misimu iliyopita. katika usajili mdogo wa january Van Persie aliuzwa na klabu yake baada ya Arsenal kufika dau la paundi millioni 2.75
      Tarehe 17 May 2004 Van Persie alisaini mkataba wa miaka minne na Arsenal. Kocha mkuu  Arsene Wenger alipanga kumbadilisha Van Persie toka winga ya kushoto na kumweka kuwa mshambuliaji wa kati kama alivyofanya kwa Thierry Henry mchezaji wa zamani wa Arsenal, alifanikiwa

      Alikaa sana benchi kwa kipindi cha 2004/2005, alifanikiwa kupata magoli 8 ndani ya mwezi mmoja mwaka 2005 na kutunukiwa zawadi ya kuongezewa mkataba mwingine hadi 2011 January 4, lakini siku mbili baadae alivunjika kidole alipokuwa anacheza fainali za kombe la FA dhidi ya Cardiff.

       Katika medani za kimataifa alifanikiwa kuiongoza vizuri timu yake ya Taifa ya Uholanzi mwaka 2006 katika fainali za kombe la Dunia. aliipa ushindi wa kuingia kumi na sita bora kwa goli lake la pekee alilofunga dhidi ya Ivory Cost. hata ivyo timu iliishia katika raundi hiyohiyo!!
      
       Tarehe 13 June 2005 akiwa na timu yake  ya taifa, Van Persie  alikamatwa kwa tuhuma za ubakaji na muhusika mkuu alikuwa Sandra Krijgsman aliyekuwa Miss Nigeria Holland, hivyo alikaa rumande kwa wiki 2 kisha kumwachia kutokana na ushahidi kutokukamilika lakini uchunguzi ulikuwa unaendelea

      February 2006 kesi iliisha na kufutwa na mahakama ya Jamhuri ya Uholanzi baada ya uchunguzi kukamilika na kukuta hakuna hatia juu ya tuhuma zilizokuwa zinamkabili mchezaji huyu.

     2012 imeingia katika historia mpya kwa Arsenal kumkosa tena mshambuliaji tegemezi aliyeihama timu hiyo na kwenda Manchester  United kwa ada ya paundi millioni 24. hapa tena hakuna mjadala.........!!!
  Swali ni je kuuzwa kwa Robin Van Persie ni  maana ya kwamba timu ya Arsenal haiwezi tena kushindana na klabu kumbwa duniani???

HII INAWAHUSU MASHABIKI WA ARSENAL !!!!   
      
Lema amwomba Slaa agombee Arusha Mjini


Godbless Lema
CHADEMA YACHANGISHA FEDHA KUNUNUA HELIKOPTA , VIJANA WAONGOZA JAHAZI 
Raymond Kaminyoge 
MBUNGE wa zamani wa Arusha Mjini, Godless Lema amesema anatamani Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa agombea ubunge wa jimbo hilo akieleza anaamini atatoa mchango mkubwa zaidi kwa chama kabla ya mwaka 2015.Lema  alitoa kauli hiyo juzi usiku jijini Dar es Salaam, wakati wa harambee ya kuchangia chama hicho kwenye kampeni yake ya Vuguvugu la Mabadiliko maarufu kama Movement for Change (M4C) mkoa wa Dar es Salaam.
mwenyekiti wa Chadema Taifa akimtambulisha Joshua Nassari mbunge wa Arumeru mashariki katika harambee ya M4C Iliyofanyika Serena Hoteli

Alisema katika chama hicho kuna watu wengi wanaoweza kuwa wabunge wa jimbo hilo, lakini yeye binafsi angependa Dk Slaa awe mbunge wa Arusha Mjini kwa sababu Katibu Mkuu huyo wa Chadema  akiwa bungeni ni moto wa kuotea mbali.

Lema alisema: “Kuhusu ubunge wa Arusha sina hofu, atakuja Dk Slaa au mimi, ingawa sasa napenda aje Dk Slaa.”
Alisema angefurahi kama Dk Slaa angekuwa mbunge wa jimbo hilo hasa katika kipindi hiki cha kutafuta mabadiliko kumpokea  wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Lema alisema hivi sasa anafurahia mchango mkubwa anaoutoa katika chama chake akiwa nje ya Bunge.
“ Nahisi kutoa mchango mkubwa katika chama nikiwa nje ya Bunge kuliko nilivyokuwa bungeni kwa sababu nimefanya shughuli nyingi zenye matokeo chanya katika taifa hili,” alisema Lema.

 Lema alienguliwa ubunge mwaka huu na Mahakama ya Kuu Kanda ya Arusha kwa kilichoelezwa kuwa alitumia lugha chafu katika kampeni za kuusaka ubunge huo mwaka 2010.

Kuchangia fedha za M4C
 Lema alieleza kuwa fedha zitakazopatikana katika harambee hiyo zitatumika kununulia helikopta, magari, pikipiki, baiskeli na matumizi mengine ya Chadema kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa ukombozi kwa wananchi.

“Tusifanye siasa ili kutafuta vyeo bali  tulenge kuleta mabadiliko chanya katika jamii iliyonyanyasika kwa muda mrefu. Nchi yetu ilipata uhuru, lakini sasa tunahitaji mabadiliko yanayowakomboa wananchi kutoka kwenye umasikini,” alisema Lema.

Kauli ya Mbowe
Akizungumza katika harambee hiyo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kuwa, propaganda za ukabila, udini na rangi zinazoenezwa na CCM ni dhaifu na zimeshindwa kuidhoofisha Chadema.

 Alisema kuwa wananchi wamezishtukia propaganda hizo na kwamba, wananchi wengi wamehamasika kutaka mabadiliko.
 Katika harambee hiyo zaidi ya Sh270 milioni zilipatikana, kati ya hizo Sh250 milioni zikiwa ni ahadi na Sh20 milioni zikiwa ni fedha taslimu.
Kati ya fedha hizo, Sh20 milioni zilichangwa na tawi la Chadema nchini Marekani likiwa na majimbo yake Washington DC, Maryland na Virginia.

 Watendaji wa Serikali
Kivutio kikubwa kilikuwa kwa baadhi ya watendaji wa Serikali kuchangia katika harambee hiyo na kutaka waitwe Wasamaria wema bila kutaja majina yao.

Mbowe alisema: “Kwa kuwa wananchi wametuamini, tumeacha njia ya maandamano na sasa tunataka kufika kila kata ya nchi hii ili kufikisha ujumbe wa mabadiliko kwa wananchi. "

Alisema kuwa wamekubaliana baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge wabunge wote wa Chadema watasambaa nchi nzima kueneza Vuguvugu la Mabadiliko.
 Mwenyekiti huyo wa Chadema alisema kuwa mbali ya kufika kwenye kila kata chama hicho pia kimejipanga kufikisha ujumbe huo katika nchi zote ambako kuna Watanzania.

“ Hatuna mchezo sasa, tumejipanga kuchukua dola ifikapo 2015, hawa CCM sasa ni kama wanaweweseka hawajui wanalolifanya, tutawang’oa tu, ” alisema Mbowe.

  Alisema kuwa chama hicho kikifanikiwa kuchukua dola, kipaumbele kikubwa kitakuwa ni kuboresha elimu ambayo ni sekta muhimu kwa maendeleo ya taifa.

“ Kipaumbele namba moja, mbili hadi tatu kitakuwa ni elimu. Tutawekeza zaidi kwenye elimu ili kuwawezesha wananchi kuhimili changamoto za dunia ya sasa hasa katika usimamizi wa rasilimali zao,” alisisitiza Mbowe.
 Aliwahimiza watu wanaokichangia chama hicho kwa kuficha majina yao kuacha hofu akisema: “Jitokezeni hadharani, hamna sababu ya kuhofu kama kweli mnahitaji mabadiliko. Tumepuuzwa, tumenyanyaswa na tumedhalilishwa kiasi cha kutosha, sasa basi tuache woga.”

Alisema kuwa, CCM imeshindwa kuwasikiliza madaktari, walimu na wafanyakazi wengine lakini Chadema inaahidi kushughulikia matatizo ya makundi hayo.
  Akizungumzia umuhimu wa harambee hiyo, Mbowe alisema mabadiliko yana gharama zake na kwamba wadau ndiyo wanapaswa kuchangia chama hicho.
Mbowe aliomba kila mpenda mabadiliko kuchangia kwa kadri ya uwezo wake na kwamba fedha zake zitailetea mabadiliko nchi hii.

Vyeo
Akizungumzia suala la nafasi za uongozi ndani ya chama hicho, Mbowe alisema kuwa, huu si wakati wa kugawana vyeo wala kutangaza nafasi za kugombea bali kukiimarisha chama ili kiweze kuwa na nguvu zaidi.
Naye Mwenyekiti wa M4C, Mkoa wa Dar es Salaam, Alex Mayunga alisema harambee hiyo  ilikuwa na lengo la kukusanya Sh5 bilioni katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema katika hafla ya jana walipanga kupata Sh500 milioni, lakini hazikutimia kutokana na msongamano wa wananchi waliokuwa wakituma fedha kwa njia ya simu za mkononi.

“Tunadhani hadi kesho (leo) kiasi hicho kitatimia kwa sababu wananchi wengi wametuma fedha lakini bado hazijatufikia,” alisema Mayunga.
 Aliwataka wananchi kutuma fedha kwa kutumia njia ya simu za mkononi  kwa sababu hiyo ndiyo njia rahisi.   Mwisho

z