Oct 21, 2012


TAHADHARI KUHUSU MABOMU 30 TOKA MALAWI

Kuna taarifa kwenye mitandao ya simu inayoendelea kutolewa kwenye message za simu kwamba  kuna Mabomu zaidi ya 30 yenye uzito usiopungua tani 100 na kuwataka wananchi katika mikoa ya Tanzania iliyo jirani na Malawi kuwa waangalifu.
Taarifa hiyo imetaka wenye wasiwasi kuhusu taarifa hiyo wapige simu 0756000042. Taarifa hiyo imedai kwamba imetolewa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Tunapenda kutoa taarifa kwamba taarifa hizo siyo za kweli na lengo lake  haliwezi kuwa zuri kwa Watanzania.

 Wananchi wanashauriwa kutotuma taarifa zozote kwenye namba hiyo ama kuziamini taarifa za aina hiyo.


Assah Mwambene
Mkurugenzi, Idara ya Habari Maelezo.

BOB HAISA AKANUSHA KUWA YEYE SIYO CHIZI KAMA WATU WANAVYODAI






















Hii picha imesambaa kwenye mtandao wa Facebook ikimwonesha Bob Haisa akiwa kama chizi na kuzua maswali mengi kama ni kweli ama ni harakati tu za kufanya sanaa.Baada ya kuona kuwa kila mmoja anazungumza lake, mwandishi wa habari hii  amemtafuta Bob Haisa ambaye baada kucheka sana aliposikia jinsi watu wanavyoizungumzia picha hiyo, amesema hiyo picha ni ya video ya wimbo wake mpya uitwao ‘Wa Kukaya’

“Safari hii sikupenda kuweka madancers kwenye video, nimeamua kuigiza mwenyewe kama Pedeshee, Choka Mbaya nk."

Amesema video hiyo bado ipo kwenye hatua za mwisho kumalizika ili itoke.