Sep 13, 2012

Ufunguzi Wa Jengo Jipya La Afisi Ya Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu Wa Hesabu Za Serikali Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohd Shein akikata Utepe kuashiria Ufunguzi wa Jengo Jipya la Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali huko Maisara Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohd Shein akitoa hotuba katika Ufunguzi wa Jengo jipya la Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali huko Maisara Mjini Zanzibar.
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Fatma Mohd Saidi akitoa hotuba katika Ufunguzi wa Jengo jipya la Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali huko Maisara Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hisabu Zanzibar wakiwa katika Hafla ya Ufunguzi wa Jengo lao Jipya huko Afisini kwao Maisara Mjini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohd Shein akipata maelezo kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Fatma Mohd Saidi kuhusu namna ya kazi zitakavyofanyika ndani ya Jengo jipya la Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali huko Maisara Mjini Zanzibar.

Waziri Mkuu Wa Zamani Misri Afungwa Jela

Mahakama nchini Misri imemhukumu kifungo cha miaka mitatu gerezani waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Ahmed Nazif.Nazif amehukumiwa baada ya kupatikana na hatia ya kosa la ufisadi.

Bwana Nazif, ambaye alikuwa waziri mkuu kuanzia mwaka 2004 hadi mwaka jana wakati mapinduzi ya kiraia yalipofanyika, pia ameamrishwa kulipa faini ya dola milioni 1.5.
Mwaka jana Ahmed Nazif alifutwa kazi kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kushtakiwa kwa kosa la kupata faida haramu kutokana na biashara alizofanya kinyume na sheria.

Nazif alikuwa mmoja wa maafisa wakuu katika serikali ya rais wa zamani Hosni Mubarak.Alikamatwa miezi kadhaa baada ya kuacha kazi mwezi Januari mwaka 2011, muda mfupi kabla ya rais Mubarak kuachia ngazi.

Maafisa kadhaa wa uliokuwa utawala wa Mubarak wamefikishwa mahakamani kwa aidha kosa la njama ya kuwaua waandamanaji au makosa kuhusiana na ufisadi.Mubarak alihukumiwa kifungo cha maisha jela mwezi Juni baada ya kuhusishwa na mauaji ya waandamanaji.