STEVEN GERRARD
Steven Gerrard alizaliwa tarehe 30 may, 1980 Whiston, Merseyside. Mji upo umbali wa km 8 mashariki ya jiji la Liverpool. Maisha yake ya utotoni yalikuwa mji wa jirani Huyton.
Gerrard au steve G kama anavopenda kujiita, ni kiungo mchezeshaji katika soka na anaweza kucheza nafasi yoyote. Anapenda sana kukimbiza na kuibua mipira iliyokufa kisha kucheza kama striker ikiwa ni pamoja na kupiga mashuti ya mbali nan i mkabaji mzuri sana kiasi cha watu wengi kupenda kucheza naye na makocha wengi kupenda kucheza naye.
Gerrard aliudhuria shule ya kadinali Heenan katoliki, West Derby, Liverpool. Pamoja na kuwa Owen, Robbie Flowler, Jamie Carragher na wachezaji wengine maarufu ambao Gerrard alikuwa nao tangu wapo Everton Gerrard aliihama timu yake hiyo na kwenda katika timu aliyoipenda ya Liverpool akiwa bado mwanafunzi! Aliinuka kwa kishindo alipoingia kucheza akitokea benchi Norwegian Vegard Heggem alitoka nje mechi na Blackburn tarehe 30 novemba 1998. Ligi ya mabingwa ulaya ilizidi kumwinua na kumweka kwenye chati alipoonesha mchezo mzuri dhidi ya Celta Vigo.
Mwaka 2000 aliitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England, mechi yake ya kwanza alicheza na Ukraine uwanja wa Wembley ambapo alionesha soka zuri sana lililowakosha mashabiki. Goli lake la kwanza lililoingia kwenye magoli mazuri ya mwaka ni pale alipopiga shuti kali lililomshinda Oliver khan wa timu ya taifa ya Ujerumani mnamo septemba 2001. Alipata majeraha ambayo yalimfanya ashindwe kucheza fainali za kombe la dunia zilizofanyika korea na Japan.
Alipewa u naodha wa klabu October 2003 na Gerard Houllier na aliiweza kazi vizuri hijawahi kutokea. Liverpool alivaa jezi namba 8 na no. 4 kwa timu yake ya taifa. Alipewa unaodha katika timu yake ya taifa na mnamo mwaka 2004 na kukutana na timu ya taifa ya Sweden. Steve Mclaren alipoichukua timu ya taifa toka kwa Sven Goran Eriksson August 2006, akampa Gerrard kuwa makamu wa naodha. Pamoja na hayo hakuaribu chochote alicheza mpira na mashabiki kujikuta wanampa kuwa ndiye mchezaji wa mwaka 2007.
Gerrard alipata magoli kwa kila mechi kubwa muhimu alizokuwa anacheza na timu yake ya Liverpool na kuonesha kwamba yeye kiwango kipo. Moja ya mechi muhimu ni pamoja na mechi waliyocheza na AC Milan ligi ya mabingwa ulaya 2005. Pia alikuwa mfungaji magoli katika mechi za ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Alves 2001 na fainali dhidi ya maadui wao wakubwa Manchestar United, Olympiakos pia hawatokuja kumsahau kijana huyo katika mashindano hayohayo!
Alizidi kupata mafanikio zaidi alipokuwa akicheza pamoja na Fernando Torres na kufanya wacheze kitimu zaidi alimaliza msimu akiwa na magoli 20. Ndie kiungo mchezeshaji aliyebaki juu kwa muda mrefu sana na kumfanya mkurugenzi mkuu Rick Parry kumwongeza mkataba mwingine hadi 2011
Gerrard ameshinda baadhi ya tuzo huko ulaya ikiwemo ya Uingereza kama mchezaji bora mwenye umri mdogo 2001, mchezaji mwenye thamani kubwa ligi ya mabingwa 2004-05 na mchezaji bora wa mwaka 2006 wakifuatiwa na Frank Lampard na Thierry Henry. Alishika nafasi ya tatu kwa mchezaji bora wa mwaka kwa nchi za Ulaya mbele ya Ronaldinho na Lampard 2005. 2006 alifanywa kuwa mjumbe wa MBE kwa mchango wake katika soka. Kwa muda wa miaka mitano mfululizo hakufeli kuwa mwanasoka bora mwaka Uingereza
Ameoa, mke wake anaitwa Alex Curran tarehe 16 June 2007 na
wana watoto wawili Lily-Ella na Lexie.