Oct 9, 2012


MWANAFUNZI AFANYA MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO CHA 4 AKIWA WODINI MOROGORO



Mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Alfa Germ, Morogoro, Jesca Kiliani (17) akifanya mtihani wa taifa akiwa wodi namba 7B  katika hospitali ya rufaa ya mkoa huo jana, baada ya kulazwa kufuatia kufanyiwa operesheni ya uvimbe.


MWANAFUNZI wa kidato cha nne katika Sekondari ya Alfa Germ, Morogoro, Jessica Kiliani (17), amelazimika kufanya mtihani wake wa kuhitimu elimu  hiyo akiwa wodini baada ya kufanyiwa upasuaji.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya mwanafunzi huyo, kuomba aruhusiwe kufanya mtihani huo licha ya kuwa  wodini akiugulia maumivu ya upasuaji aliofanyiwa na madaktari wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa zaidi ya saa mbili na kulazwa katika wodi ya wazazi namba 7B.

SKENDO CHAFU ZAMTOA MACHOZI MONALISA






MSANII nguli anayefanya vizuri kwenye tasnia ya filamu bongo Monalisa, amefunguka na kudai kuwa huwa anatokwa na machozi pale anapoona wasanii wengine wa tasnia hiyo wanafanya mambo ambayo yanaipelekea fani hiyo kuonekana ya kihuni.

Msanii huyo unaweza kusema ni moja kati ya nyota wanaofanya filamu za viwango vya kimataifa, na ndiyo maana ameweza kufika mbali ikiwemo kuingizwa kwenye tuzo kubwa kubwa za kimataifa.

Monalisa alisema kuwa mara nyingi huwa anashindwa kuelewa ni kitu gani kinachosababisha msanii kufanya mambo ya ajabu badala ya kutulia na kubuni vitu vya kufanya kwa faida ya taifa na tasnia kwa ujumla, wasanii wa nje wanapata umaarufu kupitia kazi zao ambazo zinadumu sokoni kwa muda mrefu kutokana na umakini wao.

“Kila msanii anajua anafanya nini kwenye tasnia hii lakini wote kwa pamoja lazima tujue kwamba hakuna filamu ambayo tunaweza kusema imetikisa dunia kutoka Tanzania, hivyo tunajukumu kubwa la kubuni vitu ili nchi yetu ifike mbali kupitia filamu, lakini wasanii wetu hawafikilia kitu kama hicho,” alidai.

Aliongeza kuwa kuna mitazamo feki ndani ya tasnia hiyo kuwa msanii hawezi kuwa maarufu bila skendo ambapo kwa upande wake anaamini hiyo haina maana kwa kikubwa kinachoweza kumtangaza msanii ni kufanya kwa nzuri.