Stori: Hamida Hassan na Imelda Mtema
MSANII wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’, mwanzoni mwa wiki hii alimshangaza (surprise) mama wa mpenzi wake wa zamani, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa wakati alipokuwa akisherehekea miaka 58 tokea alipozaliwa.
Keki aliyoleta Lulu kwa ajili ya mama Kanumba.
Kumshangaza huko kumekuja baada ya Lulu
kufika nyumbani kwa mama Kanumba, Kimara Temboni jijini Dar akiwa na bonge la
keki, jambo ambalo mama huyo hakulitarajia.…Stori: Hamida Hassan na Imelda Mtema
MSANII wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’, mwanzoni mwa wiki hii alimshangaza (surprise) mama wa mpenzi wake wa zamani, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa wakati alipokuwa akisherehekea miaka 58 tokea alipozaliwa.
Keki aliyoleta Lulu kwa ajili ya mama Kanumba.
Kumshangaza huko kumekuja baada ya Lulu
kufika nyumbani kwa mama Kanumba, Kimara Temboni jijini Dar akiwa na bonge la
keki, jambo ambalo mama huyo hakulitarajia.
Lulu akimpatia keki mama Kanumba.
“Yaani mama Kanumba alikuwa hajui kuwa Lulu
anajua siku yake ya kuzaliwa, Lulu akatumia nafasi hiyo kumfanyia ‘sapraizi’,”
alisema rafiki wa karibu wa Lulu aliyeomba hifadhi ya jina lake.
...Lulu akimlisha keki mama Kanumba.
Waandishi wetu waliokuwa eneo la tukio
walimshuhudia mama Kanumba akiwa amepigwa na butwaa huku akilengwalengwa na
machozi ya furaha. Mahojiano yalifanyika Ijumaa: Hongera mama, sasa unatimiza miaka mingapi?
Mama Kanumba: Nimetimiza miaka 58.
Mama Kanumba akimlisha keki mama mzazi wa Lulu, Lucresia Karugila.
Ijumaa: Umejisikiaje kwa zawadi ya keki
uliyoletewa na Lulu?Mama Kanumba: Nimejisikia furaha sana kwa kweli, Lulu ni mwanangu, nimefarijika, kwa sababu watoto wangu hawapo, leo ningekuwa peke yangu lakini kama unavyoona, mama na mwanaye wamekuja toka asubuhi tunasherehekea nao kwa kula na kunywa na Lulu amegharamia kila kitu.
Baada ya swali
Kutoka kushoto: Flora Mtegoa, Lulu na Lucresia Karugila katika
pozi.
Ijumaa: Ulijuaje leo ni siku ya kuzaliwa ya
mama Kanumba?Lulu: Nilijua katika maongezi siku sita zilizopita, kwani ilikuwa ni tarehe moja ya mwezi huu ambapo amezaliwa mama yangu mzazi na dada yangu.
Ijumaa: Kwa nini uliamua kumfanyia Sapraizi ya keki mama Kanumba?
Mama Kanumba akikata keki.
Lulu: Niliamua kumfurahisha kwa sababu ni
siku yake ya kuzaliwa na sikufanya kwa sababu mwanaye hayupo, hata angekuwepo
ningemfanyia tu.Ijumaa: Asanteni, mama na Lulu tunawatakia maisha mema.
Flora Mtegoa akipozi na Lulu.
No comments:
Post a Comment