Sep 16, 2012

MJUE STAR WETU WA LEO (GREAT)!!

Maisha ya Yesu kwa ujumla yameelezwa katika vitabu vya agano jipya, Mathayo, Luke, Marko na Yohana. hawa wote wanatoa historia zinazoelekeana lakini yote ni kuwaleta wakristo ulimwenguni kote katika imani moja ya kuamini kwamba Yesu ndiye mtu pekee aliyekuja duniani na kuondika na dhambi za wanadamu.
      Yesu alizaliwa miaka 2000 iliyopita katika mji wa Bethelehemu, Uyahudi. Bikira Maria ndiye mama mzazi wa Yesu, wakati Yusufu ndiye baba mzazi wa Yesu wa kufikia maana ndiye alikuwa mchumba wa Mariam lakini mimba aliipata kwa uweza wa roho mtakatifu. Yusufu alikuwa ni fundi selemala hivyo Yesu pia alikuwa anafuata nyayo za baba yake.
       kutoka katika kitabu cha mtakatifu Mathayo 2:1 Yesu alizaliwa kipindi cha uongozi wa mfalme Herode wa kwanza, ambaye alipopata habari za uzao huo na kusikia kwamba ataweza kuwa mfalme wa baadae akatoa amri ya kuuawa kwa watoto wa kiume wabetherehemu. Yusufu alipewa taarifa na malaika toka mbinguni na kumwambia akimbie katika mji ule yeye na familia yake. alienda Misri, walikaa huko mpaka waliposikia Herode amefariki ndipo wakarudi Nazareth, galilaya.
       Historia ya Maisha ya Yesu imeandikwa kidogo sana. Injili ya Luka (2:41-52) anaeleza kwamba Yesu alipofika umri wa miaka 12 akiwa na wazazi wake aliwatoroka na kukimbilia moja ya nyumbba walizotumia kuabudia Yerusalemu. walimtafuta kwa siku kadhaa baadae wakamkuta katikati ya wazee wa kanisa akisikiliza na kuchangia mada. walimshangaa sana kwa mtoto mdogo kama yule kutoa maneno ya busara kwa kiasi kile.
        Alianza kazi ya kuhubiri akiwa na miaka 30 pale tu alipobatizwa nan Yohana ambaye alipomwona tu aligundua kwamba huyu ndiye mwana wa Mungu.
       Baada ya Yesu kubatizwa alikwenda jangwani na kufunga kwa siku 40 usiku na mchana. akiwa huko shetani alienda kumjaribu, majaribu hayo yanapatikana katika Mathayo, Marko na Luke. Yesu alijaribiwa mara tatu ikiwa ni kugeuza jiwe kuwa mkate, kujirusha toka kwenye mnara mpaka chini malaika zake waje kumdaka, na tatu ni kumwahidi kumpa falme na utajiri wote wa dunia. Lakini Yesu alifanikiwa kuyashinda majaribu yote.

itaendelea wiki ijayo kwa siku kama hii kuteswa, kufa na hata kufufuka kwake.........!!! tafakari ukuu wa Mungu  leo..

No comments: