Oct 26, 2012

MJUE STAA WETU WA LEO!

Obama,_BarackBarrack Hussein Obama II alizaliwa tarehe 4 August 1961 mama mwenye asili ya kizungu nchini Marekani, Ann Dunham na baba wa kiafrika mwenye asili ya Kenya, Barrack Obama Sr. Ann na Barrack walipata motto wao wakiwa bado ni wanafunzi wa chuo kikuu cha Hawaii. Barrack Hussein aliondoka nchini Marekani na kurudi Kenya akawa mchumi wa serikali, huku nyuma akimwacha mwanae na mama yake. Ann aliolewa na mwanaume mwingine raia wa Indonesia aliyekuwa manager wa kampuni ya mafuta (oil), Jakarta Barrack akiwa na umri wa miaka sita. Barrack aliona maisha ya Indonesia ni magumu hivyo alilazimika kurudi nchini Marekani kuishi na babu yake aliyekuwa anafanya biashara ya samani za ndani wakati bibi yake alifanya kazi benki. Familia iliishi katika nyumba za kupanga, pamoja na kipato kidogo walichokipata waliweza kumpeleka shule iliyokuwa juu katika mji wa Hawaii. Alionana na baba yake akiwa ametimiza miaka kumi.

Alijiunga na chuo kikuu cha Columbia, alikutana na ubaguzi wa rangi umetapakaa New York. Alikuwa kiongozi wa jumuiya wa kanisa moja Chikago kwa miaka 3, akisaidia watu masikini wasio na makazi maalum. Baadae alijiunga na chuo kikuu Havard kusomea sharia, mwaka 1990 alikuwa mwafrika wa kwanza mhariri wa mapitio ya sharia. Pia alianza kufundisha chuo kikuu Chicago kitivo cha sharia na baadae kuoa Michelle Robinson aliyekuwa mfanyakazi mwenzie.

Mwaka 2004 Obama alichaguliwa kuwa Seneta akiwakilisha IIlinois, wananchi walipata hamasa ya kendelea kumfahamu Barrack alipohutubia mkutano wa chama cha demokrasia, Boston. Mwaka 2008 aligombea urais, pamoja na kwamba alikuwa kwenye siasa kwa miaka 4 alishinda kiti cha urais. Mwaka 2009 january aliapishwa kuwa rais wa 44 wa Marekani na kuwa mwafrika wa kwanza kuingoza Marekani.

Alishauliwa na mkewe kuacha kuvuta sigara kutokana na kampeni alizofanya za kugombea urais na yeye kutii na kuacha kabisa.




No comments: