Oct 8, 2012


MSANII WA BONGO MOVIE AAMUA KUJICHORA TATOO KATIKA MAKALIO YAKE





















MSANII ndani ya tasnia ya filamu na tamthilia za kibongo Rayuu amezidi kujichora tattoo kwenye mwili wake ambapo sasa aamua kuchora kiunoni na sehemu  nyingine nyeti.  Mtandao huu  baada ya kusikia taarifa hizo kutoka kwa rafiki yake kipenzi kuwa msanii huyo amezidi kujichafua mwili kwa kujichora ndipo ulipoamua kumtafuta ili kupata ukweli wa ishu hiyo na alipopatikana alifunguka kuwa ni kweli lakini zote alizochora hazina ubaya wowote.Rayuu alisema kuwa amechora michoro hiyo sehemu nyingi za mwili wake kuanzia kiunoni, shingoni, kwenye maziwa, makalio na mapaja na alidai kuwa anajisikia...furaha kuwa na tattoo hizo kwani hajafanya kwa kushawishiwa na mtu.

Alidai kuwa hata hivyo kati ya michoro hiyo aliouweka kiunoni unasomeka jina lake la 
 ‘Rayuu’ na mengine ni ya aina mbalimbali,“tattoo nazipenda sana lakini kati ya zote hii ya kiunoni naipenda kuliko zote ingawa aliyenichora aliikosea kidogo,”alisema.
Related Posts Widget For Blogger with ThumbnailsBlogger Templates

" MUZIKI UMENITENGA NA WAZAZI WANGU"....LINAH


KIMWANA ambaye hivi sasa yupo kwenye mahusiano na jamaa ambaye anayeishi nchini Marekani, Linah Sanga, amedai kuwa huwa anapoenda nyumbani kwa wazazi wake huwa navaa nguo ndefu tena za kilokole zaidi ili asije kuwaudhi wazazi wake ambao wamemkuza katika maisha hayo. Msanii huyo anapenda kuishi kizungu baada ya kuigia kwenye muziki, ingawa anadai kuwa hawezi kusahau maisha ya kidini aliyokuwa anaishi awali ambayo yalikuwa yanamfanya avae nguo za heshima tofauti na sasa. Linah alidai kuwa tangu alipoachana na wazazi wake maisha yake yamekuwa tofauti kwani muziki kwa upande fulani umebandilisha maisha yake, kuanzia kwenye mavazi tabia na hata lifestyle.

“Napozungumza tabia haimanishi nimekuwa muhuni hapana, bali awali nilikuwa sijuani na watu maarufu lakini sasa nimekuwa nao karibu na kuna baadhi ya vitabia nimekuwa navyo lakini si kwa ubaya,” 
alidai na kuongeza

"Na  ninapoenda  kuwaona  wazazi  hunilazimu  nivae  kilokole  maana  sipendi  kuwakwaza"



Msanii huyo aliongeza kuwa wazazi wake wamekuwa wakimsihi sana kuvaa nguo zile zile za zamani lakini haoni kama zina nafasi kwa sasa kutokana na career aliyoichagua.

MWANA FA AMWAGIWA "MAMILIONI" YA SIFA BAADA YA KUFUNIKA KATIKA SHOW YA FIESTA


Kwa kujiamini kabisa, tunasema haijawahi katika historia ya Fiesta na show za muziki wa Tanzania msanii kusifiwa kwa kazi nzuri aliyoifanya kwenye stage kama ilivyokuwa kwa Mwana FA!  Huenda sababu ikawa ni kukua kwa mitandao ya jamii kama Twitter ambapo mashabiki wana nafasi rahisi kutoa pongezi zao kwa msanii husika lakini seriously Mwana FA aka Binamu aliangusha performance kali pengine kuliko zote alizowahi kuzifanya kiasi cha jana kwenye Twitter kugeuka mjadala na hata kuifunika show ya Rick Ross ambayo nayo ilikuwa kali sana. Mwana FA aliingia stejini kwa plan nzuri ya namna ya kuimba nyimbo zake. Tunahisi alifanya rehearsal na maandalizi ya maana. 

Akiwa na T-shirt nyekundu yenye maandishi ‘CAN’T STOP THE HUSTLE & GRIND na miwani iliyokuwa na mishikio yenye rangi nyekundu pia, alionekana smart kinoma.
FA alikuwa ameandaa nyimbo zaidi ya sita zilizohit kinoma na kuchagua kuziimba verse moja moja huku kila moja ikishangiliwa na mashabiki. Kwa kujiamini, FA aliyekuwa mcheshi muda wote aliweza kuongea na mashabiki kuliko msanii yoyote aliyepanda siku hiyo isipokuwa Rozay tu. 

‘Zipo nyingi, sasa ntafanyeje?’ alisikika FA mara nyingi baada ya kuwa anakatisha nyimbo zake ili kuimba nyingine.

 Unanitega, Mabinti, Binamu, Yalaiti, Habari Ndio Hiyo, Unajinua Unasikia, Naongea na wewe na zingine ziliamsha shangwe za wengi kwenye viwanja vya Leaders. 

Akiongea leo kwenye kipindi cha Power Breakfast kutoa shukrani kwa wananchi kwa jinsi walivyoiunga mkono Fiesta, mkurugenzi mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kussaga, amesema wapo wamarekani waliomfuata na kumuuliza ‘who is that guy’ wakati FA alipokuwa kwenye stage.

Kwa namna yoyote ile, performance hiyo ya aina yake ya rapper huyo ambaye jina lake halisi ni Hamis Mwinjuma, imefungua ukurasa mwingine mpya wa heshima aliyonayo ndani na nje ya nchi na huenda ikampa michongo mingi zaidi. Kiukweli FA, amelitumia vema jukwaa la Fiesta na huo ndio tunauita ‘ukomavu’.

Hizi ni baadhi ya tweets zilizokuwa zikisifia show ya Mwana FA.

No comments: