Oct 11, 2012


DIAMOND AJISIFU KWA KUYAANIKA MAKALIO YAKE.....ADAI KUWA HUO NI UBUNIFU ULIOMPA UMAARUFU ZAIDI


 DUNIA INA MAMBO....BADALA YA KUWAOMBA  RADHI MASHABIKI, MSANII DIAMOND  NDO KWANZA AMEFUNGUKA NA  KUDAI KUWA  KUVUA  BOXER  KUMEMFANYA  AWE  MAARUFU ZAIDI.........

 NAOMBA  KUMNUKUU TOKA KATIKA WEB YAKE:

"First of all ningependa sana kutanguliza shukrani zangu kwa Mwenyezi Mungu kwa muda huu wote wa kuusimamia na kuuongoza muziki wa Bongo Flavour kuanzia umeanza hadi leo ulipofikia...

Kiukweli umepiga hatua kubwa sana,kadri siku zinavyozidi kwenda ndipo muziki huu umekua ukizidi kupata Umaarufu,kupata Mashabiki na kufatiliwa ndani na nje ya nchi...

Honestly najivunia sana kuwa mtanzania na kuwa Miongoni mwa Wanabongoflavour hao....

Na hii ni moja ya show Kali ambayo kiukweli katika hii wiki imezua gumzo sana,sifa na kufanya ulimwengu kutaka kuzidi kuufahamu na kuujua muziki wa bongo flavour zaidi kutokana na ubunifu uliofanyika humu ndani ......" DIAMOND

No comments: