HITILAFU YA UMEME YASABABISHA VIFO VYA MWANAMKE MMOJA NA WANAWE WAWILI.
Sehemu
ya masalia ya vyombo na samani zilizoteketea kwa moto kufuatia hitilafu
ya umeme iliyopelekea mama mmoja na wanawe wawili nao kutoketea katika
Mtaa wa Mapelele,Kata ya Ilemi Jijini Mbeya.
Nyumba iliyoteketea kwa moto baada ya hitilafu ya umeme.
*******
Mwanamke
mmoja mkazi wa mtaa wa Mapelele kata ya Ilemi Jijini Mbeya amefariki
dunia akiwa amelala chumbani na wanawe wawili baada ya moto mkubwa
kuzuka uliosababishwa na hitilafu ya umeme majira ya saa 4.55 usiku
agosti 16 mwaka huu wakati familia hiyo ikiwa imelala chumbani .
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani
Mbeya Bw. Barakiel Masaki aliwataja marehemu hao kuwa ni pamoja na
Bi.Pendo Paul (23) mkazi wa Ilemi, na watoto wake wawili ambao ni Tekla
Paul(4),Aman Paul mwaka mmoja ambao wote walikuwa wamelala chumba kimoja
wakati moto unatokea.
Alisema kuwa wakati moto huo
unatokea mume wa mwanamke huyo aitwaye Paul Mlelwa alikuwa safarini
Jijini Mwanza kikazi kwa muda wa wiki moja sasa toka aondoke na kwamba
familia hiyo imehamia katika nyumba hiyo ya kupanga mwezi mmoja
uliopita.
Akizungumzia tukio hilo barozi wa
mtaa huo Bw.Pius Mwampenjele alisema alipata taarifa za ajali ya moto
huo ndipo alipoomba msaada kwa majirani ili kuweza kusaidia kuzima moto
ambao tayari ulikuwa umeshateketeza vyumba viwili na familia ya Bw.
Paulo ambayo ilikuwa na mke na watoto wawilli waliokuwa wamelala
chumbani walishafariki dunia.
Hata hivyo Mwenyekiti wa mtaa wa
Mapelele Bw.Christopher Mwakibete alisema kwamba tukio hilo ni la pili
katika mtaa wake kwa muda wa wiki moja kufutia tukio la kwanza kutokea
agosti 14 mwaka huu ambapo watu wawili ambao ni mke na mume walifariki
dunia kwa moto uliosababishwqa na hitilafu ya umeme ambayo ilikuwa ni
majira hayohayo.
Alisema kuwa matatizo ya umeme
katika mtaa wake yamelipotiwa mara nyingi kwa diwani wa kata ya Ilemi na
ofisi za Tanesco Mkoa lakini hakuna hatua zozote ambazo zimechukuliwa
zaidi ya kutelekeza nguzo za
umeme kwa muda mrefu bila utekelezaji .
Aidha ameongeza kuwa uwezo
Transifoma umekuwai mdogo kutokana na wingi wa wateja na mara nyingi
umeme umekuwa mdogo na wakati mwingine kuzima kabisa hali ambayo
inahatarisha usalama wa wananchi wa eneo hilo.
No comments:
Post a Comment